Home BIASHARAUWEKEZAJI Maeneo ya uhifadhi ni muhimu kwa uchumi: Mchengerwa

Maeneo ya uhifadhi ni muhimu kwa uchumi: Mchengerwa

0 comment 99 views

Tanzania leo Machi 3, 2023, inaungana na nchi nyingine kuadhimisha Siku ya Wanyamapori Duniani (World Wildlife Day).

“Maeneo ya uhifadhi ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi na yanachangia asilimia 17 ya pato la taifa, asilimia 25 ya fedha za kigeni na kutoa ajira takribani 1.5 kwa Watanzania,” amesema Waziri wa Maliasili na Utalii Mohamed Mchengerwa.

Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa wadau wa uhifadhi nchini kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa rasilimali za wanyamapori zinaendelea kuhifadhiwa kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Taarifa ya Waziri Mchengerwa inasema sherehe za mwaka huu zinakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya Mkataba wa Kimataifa wa Kuthibiti Biashara ya Wanyamapori na Mimea iliyohatarini kutoweka (CITES).

Tanzania ni mwanachama wa Mkataba huo wenye jumla ya nchi wanachama 184.

Taarifa hiyo inasema “wakati tunaadhimisha siku hii ni vizuri kukumbuka kuwa Tanzania ina mchango mkubwa duniani katika uhifadhi wa wanyamapori, imetenga asilimia 32.5 ya eneo lake kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori linalojumuisha Hifadhi za Taifa 22, Mapori ya Akiba 29, Mapori Tengefu 25, Eneo la Uhifadhi ya Ngorongoro, Jumuiya za Hifadhi za Jamii 38 pamoja na Ardhioevu (Ramsar Sites) tatu.”

Aidha, amewashukuru wafadhili mbalimbali na kuwapongeza Askari na Maafisa wa Jeshi la Uhifadhi kwa kuendelea kulinda rasilimali za wanyamapori hapa nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter