Home AJIRANAFASI ZA KAZI Serikali ya Tanzania yatoa ajira mpya 21,200

Serikali ya Tanzania yatoa ajira mpya 21,200

0 comment 150 views

Serikali ya Tanzania imetangaza ajira 21,200 kwa kada za walimu na afya.

Tangazo la Serikali limetolewa na Waziri wa TAMISEMI Angella Kairuki April 12, 2023 Jijini Dodoma ambapo amesema mwisho wa maombi hayo ni tarehe 25 April, 2023 saa 05:59 usiku.

Waziri Kairuki ametaja mgawanyo wa nafasi hizo ni 13,130  ambazo zitachukuliwa na walimu wa shule za msingi na Sekondari.

Aidha idadi ya watumishi watakaoajiriwa katika kada za Afya ni 8,070 ambao watafanya kazi katika Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati.

Waombaji ni wahitimu wa nafasi hizo kuanzia mwaka 2015 hadi 2022 ambao watakuwa na sifa stahiki na wasiozidi umri wa miaka 45 lakini wanaofanya kazi za kujitolea wameitwa kuomba nafasi hizo ili waingie katika mfumo wa ajira serikalini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter