Home VIWANDAUZALISHAJI Mradi wa REGROW wataka eneo kubwa la uwekezaji

Mradi wa REGROW wataka eneo kubwa la uwekezaji

0 comment 111 views

Msimamizi wa Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) Dkt. Aenea Saanya ameushauri Uongozi wa Kijiji cha Tungamalenga kutafuta eneo lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 5 linalomilikiwa na Serikali ya Kijiji hicho kwa ajili ya kuanzisha manzuki.

Kupatikana kwa eneo hilo kutafanya mradi huo kuwa endelevu na utakaosaidia kuinua pato la kijiji na mwananchi mmoja mmoja .

Hatua hiyo inakuja kufuatia Kikundi cha ufugaji nyuki cha Subira chenye wajumbe 22 kuanzisha manzuki kwa ufadhili wa mradi wa REGROW katika eneo la mmoja wa mwanakikundi jambo ambalo linaweza kuleta mgongano wa maslahi huko mbeleni.
Kauli hiyo imetolewa mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea eneo ambalo mradi wa manzuki unatekelezwa na kikundi hicho cha Subira kilichopo mkoani Iringa.
Amesema endapo eneo hilo litapatikana timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii itafika katika eneo hilo kwa ajili ya kuangalia kama linafaa kwa ajili ya ufugaji nyuki huku akisisitiza taratibu zingine zitafuatwa kwa ajili ya kulitangaza eneo hilo la Manzuki kwenye gazeti la serikali.


Mradi huo wa REGROW unategemea kutoa milioni 20 kwa ajili ya kukiwezesha kikundi hicho cha Subira kununua mizinga 100 hivyo ni muhimu eneo hilo likatambulika kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Fredrick Funzila amemhakikishia Msimamizi wa Mradi huo kuwa litapatikana eneo linalomilikiwa na Serikali ya Kijiji kwa vile uwekezaji huo una manufaa makubwa kwa wananchi hao na Taifa kwa ujumla.

Katika ziara hiyo Msimamizi wa Mradi huo, Dkt. Saanya aliongozana na timu ya wataalamu ya ufuatiliaji wa mradi huo kutoka Benki ya Dunia na watekelezaji wa mradi wa REGROW.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter