Home BIASHARA Maonesho Sabasaba yatakuwa ya kipekee: wadau

Maonesho Sabasaba yatakuwa ya kipekee: wadau

0 comment 143 views

Wadau wa Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) Sabasaba wamesema maonesho ya mwaka huu ni ya kipee kwa kuwa yanatoa fursa kwa Taasisi, kampuni wajasiriamali na watu mbalimbali kushiriki katika maandalizi ya maonesho hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni Tanzakwanza Stragists, Francis Daudi amesema wana mabanda maalum Expo Village lengo likiwa ni kuonesha huduma zinazopatikana katika sekta mbalimbali nchini.

“Kampuni yetu kwa kushirikiana na TanTrade tumeandaa banda maalum la expovillage kwa lengo la kukutanisha sekta nane ambazo ni madini, kilimo, mazingira, uwekezaji michezo na zingine kujadili changamoto na fursa zilizopo,”amesema Francis.

Amesema SabaSaba Expo Village imelenga kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje na kuonesha rasilimali watu iliyopo nchini.

Kwa upande wake msanii wa filamu nchini Salim Ahmed maarufu kama Gabo ameeleza kuwa atakuwepo katika Banda la SabaSaba Expo
Village ambapo ataonesha filamu yake mpya aliyoitengeneza baada ya kuwezeshwa mkopo na Serikali.

Gabo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuthamini na kuwawezesha wasanii nchini.

Naye Mtafiti na Mgunduzi wa vyakula vya asili kutoka kampuni ya Dorikin, Profesa Dorcas Kibona amesema kampuni yake itakuwepo na kuonesha bidhaa zinazotokana na kilimo hai na kuwashirikisha vijana katika fursa mbalimbali zinazotona na kilimo hai.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam, Namoto Yusuph amesema wanataka kuwa na kituo maalum cha pamoja cha kuzalisha bidhaa.

“Kuna machinga wengi ni wazalishaji wa bidhaa kama batiki, sandozi na bidhaa mbalimbali tunahitaji kuwa na kituo maalum ili iwe rahisi kuwaunganisha na wataalamu namna ya kutengeneza bidhaa zenye viwango na Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS) ikague bidhaa hizo,” amesema Yusuph huku akiwaomba machinga kujitokeza kwa wingi kwenye maonyesho hayo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter