Home BIASHARAUWEKEZAJI Tanzania, Indonesia zasaini mikataba saba

Tanzania, Indonesia zasaini mikataba saba

0 comment 108 views

Serikali ya Tanzania imeridhia uamuzi wa Serikali ya Indonesia kufufua shughuli za Kituo cha Mafunzo ya Kilimo kwa Wakulima (FARTC) kilichopo Mkindo mkoani Morogoro.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo wakati akizungumza na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Joko Widodo aliyepo nchini kwa ziara ya kikazi.

Rais Samia amesema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1996 na Serikali ya Indonesia kimechangia kwa kiasi kikubwa kuelimisha wakulima na kutoa mafunzo kwa wataalamu a kilimo.

“Tanzania na Indonesia zimekubaliana kukuza biashara na uwekezaji ka kuzileta pamoja sekta za umma na binafsi ili kuimarisha ushirikiano katika viwanda, kilimo, nishati, madini, mafuta na gesi, uvuvi na utalii,” amesema Rais Samia.

Ameongeza kuwa majadiliano hayo yamebainisha nia ya Tanzania kupata uzoefu wa uzalishaji mafuta kutoka kwa Indonesia ambayo ni mzalishaji mkubwa zaidi a mafuta ya mawese duniani.

Rais Samia amesema Tanzania imejidhatiti kuhakikisha inaongeza uzalishaji wa mafuta ya kula ili iache kabisa kutumia fedha za kigeni kuagiza mafuta kutoka nje yan nchi.

Nchi hizo mbili zimetia saini hati saba za makubaliano (MoU) ikiwemo sekta za ulinzi, nishati, kilimo, mifugo, uvuvi, uchumi wa buluu, madini na pia misamaha ya viza kwa wamiliki wa hati za kusafiria za kidiplomasia na za huduma.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter