Home BIASHARA Bei za mafuta zapanda tena Tz

Bei za mafuta zapanda tena Tz

0 comment 96 views

Bei za mafuta zapanda tena Tz Bei ya dizeli yapaa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kupanda kwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli Tanzania ambapo bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ni Tsh. 3213, dizeli Tsh. 3259 na mafuta ya taa Tsh. 2943 kwa lita.

Taarifa ya EWURA imesema mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi September 2023 yanatokana na kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la dunia kwa hadi 21%, gharama za uagizaji wa mafuta hadi 62% ikilinganishwa na mwezi August 2023 na maamuzi ya kisiasa katika nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi (OPEC+).

Bei hizo kwa mkoa wa Tanga petrol ni Tsh. 3,259, dizeli 3,305 na mafuta ya taa ni 2,989.
Mtwara petroli ni Tsh. 3,285, dizeli 3,332 na mafuta ya taa 3,016.

Bei hizo zitatumika kuanzia September 06, 2023.

Itakumbukwa kuwa bei za mafuta kwa mwezi wa Agosti petroli iliuzwa Tsh. 3,199, dizeli Tshs. 2,935 na mafuta ya taa Tsh. 2,668 kwa mkoa wa Dar es Salaam. Tanga petrol iliuzwa Tsh. 3,245, dizeli 2,981 na mafuta ya taa 2,740. Kwa upande wa Mtwara petrol iliuzwa Tsh. 3,271, dizeli 3,008 na mafuta ya taa 2,714.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter