Home BIASHARA Acacia kusitisha shughuli zake Mgodi wa Buzwagi

Acacia kusitisha shughuli zake Mgodi wa Buzwagi

0 comment 155 views
Na Mwandishi wetu

Siku chache baada ya Kampuni ya Acacia kutangaza kupitia tovuti yao kuwa inatarajia kupunguza operesheni zake kwenye Mgodi wa Bulyanhulu baada ya kuzuiwa kuendelea kusafirisha mchanga wa dhahabu tangu Machi mwaka huu, kampuni hiyo imeanza kukabidhisha baadhi ya mali zake katika Mgodi wa Buzwagi kwa serikali.

Mgodi huo ambao unatarajiwa kufungwa miaka mitatu ijayo unakuwa mgodi wa pili kufungwa na kampuni hiyo baada ya mgodi wa Tulawaka ambao uliuzwa mwaka 2013 kwa Shirika la Taifa la Madini (Stamico). Kampuni ya Acacia imedai kupoteza takribani Sh. 583 bilioni katika miezi sita ambayo haijasafirisha mchanga huo.

Katika utekelezaji wa makabidhiano hayo, Acacia imekabidhi Uwanja wa Ndege uliopo katika mgodi huo kwa serikali, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Teleck amedai kuwa hatua hiyo ni ya awali katika mchakato huo wa mgodi kusitisha shughuli zake zote kwa mujibu wa mkataba uliopo.

Mbali na hayo, Acacia imetangaza mkakati wa kubana matumizi ambao utapelekea kupunguzwa kwa wafanyakazi na wakandarasi. Kampuni hiyo pia inatarajia kupunguza operesheni zake za uzalishaji kwa karati 100,000 katika Mgodi wa Bulyanhulu japokuwa bado mazungumzo kati ya serikali na Kampuni ya Barrick ambayo inamiliki asilimia 64 za hisa za Acacia bado yanaendelea.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter