Home BIASHARAUWEKEZAJI Zanzibar yahamasisha wawekezaji wazawa

Zanzibar yahamasisha wawekezaji wazawa

0 comment 228 views

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuunga mkono juhudi za wawekezaji wanaowekeza nchini kwa kusimamia misingi na sheria za uwekezaji ili kuinua uchumi wa nchi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhan Soraga amesema hayo wakati akifungua duka la vifaa vya kielektroniki.

Amesema hatua hiyo itasaidia serikali kuongeza mapato na kukuza uchumi pamoja na kuongeza ajira kwa wazawa.

“Tunaendelea kutoa mkazo kwa wawekezaji wetu wazawa kwamba hii sasa ni fursa yetu, Dola laki moja naamini wengi wetu sasa inaweza ikatupa fursa mana wakati ule Dola laki tatu ilikuwa inalalamikiwa kwamba ni kubwa sana watu wengi wanashindwa kuimudu,” amesema.

Amebainisha kuwa kwa iyo sasa serikali imeona iangalie uwekezaji wa Dola laki moja ili kuwaunga mkono wawekezaji wazawa na wao waweze kuwa sehemu ya ajenda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa MThree Investment Sekandar Ibrahim Salehe ameahidi kulipa kodi kwa wakati kuchangia Pato la Taifa.

Balozi wa Brazil Zanzibar Abdulsamad Abdulrahim amesema wataendelea kumuunga mkono Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi kwa kuhamasisha wawekezaji kuwekeza Zanzibar kwa kutangaza fursa zilizopo.

“Tutachangia kuhamasisha ndugu zetu kutoka nje, Diaspora kuwekeza akini vilevile ni kumuunga mkono Dk Mwinyi anafanya makubwa na wazawa nao wanamuunga mkono katika kutekeleza ilani ya chama na maono yake,” amesema.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter