Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof Kitila Mkumbo ametoa maagizo kwa Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kuwalinda wawekezaji hususani wa ndani ya nchi ili wasikwame katika suala la uwekezaji huku akiwaasa pia kuwawezesha pale panapostahili ili kukuza sekta ya uwekezaji nchini.
Prof Mkumbo ametoa maagizo hayo Januari 5, 2025 wakati alipotembelea kiwanda cha Mati Super brands Ltd kilichopo Kata ya Bagara ziwani wilaya ya Babati, Mkoani Manyara.
“Niwaelekeze TIC wawekezaji kama hawa muwape jicho la kipekee uwekezaji wao usikwame hata dakika moja,” amesema Prof. Mkumbo.
Aidha katika hatua nyingine Prof. Mkumbo ameitaka TIC kuwawezesha wawekezaji kwa namna yoyote ile ili kuhakikisha wanafanikisha uwekezaji wao na kuliingizia taifa kipato huku akihaidi serikali kuhakikisha mazingira wezeshi kwa wawekezaji nchini na kuahidi kuwasikiliza pindi wanapokutana na changamoto mbalimbali.
Kwa upande wake mmiliki wa kiwanda hicho amesema kuwa kiwanda chake kimeajiri wafanyakazi 269 ambapo kati yao 147 ni wa kudumu na wafanyakazi 147 ni wa muda na wote ni Watanzania.
Mulokozi ameongeza kuwa kiwanda hicho kinalipa huku huku akibainisha kuwa mwaka 2024 kiwanda kililipa kiasi cha Shilingi bilioni nane.