Home VIWANDAMIUNDOMBINU TPA kutoa huduma mtandaoni

TPA kutoa huduma mtandaoni

0 comment 110 views

Katika kuendana na kasi ya teknolojia na kurahisisha huduma kwa wateja wao, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) inatarajia kuanza kutoa huduma kidigitali kwa wateja  walio ndani na nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Deusdedit Kakoko amesema hayo wakati wa kongamano la wadau watumiao bandari ndani na nje lililofanyika jijini Dar es salaam. Kakoko ameongeza kuwa, TPA inafanya maboresho mbalimbali na itaendelea kufanya hivyo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma.

Akizungumza katika kongamano hilo, Waziri wa Usafirishaji kutoka jimbo la Kivu nchini DRC Jeo de Dion amesema wafanyabiashara wengi wanaotumia bandari ya Dar es salaam kutoka Congo wanalalamikia ushuru na mizigo kusubiri kwa muda mrefu huku gharama za matumizi ya bandari zikiwa kubwa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Ujenzi na Uchukuzi Atashasta Nditiye amesema serikali inaendelea kufanya kila linalowezekana kuhakikisha sekta ya usafirishaji hapa nchini inaboreshwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter