Home BIASHARAUWEKEZAJI Wawekezaji zaidi wakaribishwa nchini

Wawekezaji zaidi wakaribishwa nchini

0 comment 226 views

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema bado kuna uhaba wa wawekezaji hapa nchini na wawekezaji zaidi wanahitajika hasa katika sekta ya uzalishaji wa sukari ili kukidhi mahitaji ya taifa. Majaliwa amesema hayo wakati akizungumza Balozi wa Mauritius nchini Tanzania, Jean Pierre Jhumun ofisini kwake jijini Dodoma.

Majaliwa ameeleza kuwa Tanzania imebarikiwa na maeneo mengi ya uzalishaji wa sukari lakini bado hayajaendelezwa, na kutoa wito kwa wawekezaji waliokidhi vigezo kuendelea na hatua za uzalishaji. Mbali na wawekezaji wa sukari, Waziri Mkuu pia amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Mauritius kufika nchini na kuwekeza katika sekta ya uvuvi.

“Mnaweza kuja kuwekeza kwenye viwanda vya usindikaji wa samaki kwani tuna bahari, mito na maziwa yenye samaki wa aina mbalimbali”. Amesema Majaliwa.

Kwa upande wake, Balozi Jhumun amesema wamepokea wito wa Rais Magufuli wa kusaidia upatikanaji wa wawekezaji watakaowekeza kwenye viwanda kwa mikono miwili na kuongeza kuwa, wawekezaji kutoka Mauritius wapo tayari kuwekeza katika uzalishaji wa sukari na uvuvi na tayari baadhi yao wameshafika hapa nchini na kufanya utafiti katika baadhi ya maeneo kama Kasulu, Kibondo na Rufiji mkoani Pwani.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter