Home VIWANDAUZALISHAJI Tizeba aagiza SBT kuchochea uzalishaji sukari

Tizeba aagiza SBT kuchochea uzalishaji sukari

0 comment 93 views

Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba amesema serikali imeagiza bodi ya sukari nchini kusimamia majukumu yake kwa weledi na kuchochea uzalishaji wa sukari kwa wingi ili kuepukana na uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi kwani makampuni mbalimbali ya sukari ndani ya nchi yameitikia wito wa kuongeza uzalishaji ili nchi iweze kujitegemea kwa bidhaa hiyo.

Dk. Tizeba amesema hayo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) mjini Dodoma ambapo amemtaka Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari nchini, Mwamini Juma Malemi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania, Prof. Kenneth Michael Kitundu Bengesi kuhakikisha wanadhibiti sukari inayoingizwa nchini bila kufuata utaratibu na kuwataka kusimamia kwa ufasaha uongezaji wa uzalishaji wa sukari.

Kuhusu ufungashaji wa sukari kwenye ujazo wowote ule kwa kutumia vifungashio vya aina yoyote, Waziri Tizeba amesema ni lazima kuzingatia Sheria ya Sukari Namba 26 ya Mwaka 2001 inayozuia ufungashaji wa sukari bila idhini ya Bodi ya Sukari Tanzania. Kwa mujibu wa Sheria hiyo, ni marufuku kufungasha au kuuza sukari nyeupe kwani sukari hiyo ni maalum kwa ajili ya matumizi ya viwandani na sio kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

“Kuna watu wanaolipa kodi ili wazalishe sukari lakini inapoingia sukari ambayo imepenya kinyemela hata ulinganifu wa soko madukani unakuwa mdogo kwa kuwa wanaoingiza bila utaratibu wanauza kwa kiasi cha chini kwa kuwa hawana uchungu wa kulipa kodi. Na hili sio jambo la hiari Bodi ni lazima isimame kidete kubaini mianya yote ya wafanyabiashara wanaoingiza sukari bila utaratibu”. Amesema Waziri Tizeba.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter