Home VIWANDAUZALISHAJI Mgumba atangaza upungufu wa sukari

Mgumba atangaza upungufu wa sukari

0 comment 109 views

Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba amesema kwa sasa, taifa linakabiliwa na upungufu wa sukari wa zaidi ya tani 260,000, kiasi ambacho Naibu Waziri huyo amedai kinapaswa kuwa sehemu ya mahitaji ya lazima kama nchi. Mgumba ameeleza kuwa kuna upungufu wa sukari ya viwandani tani 155,000 na sukari ya mezani zaidi ya tani 105,000.

“Tumeanza ziara ya siku sita mikoani na leo (jana), tumeanzia Kilimanjaro na kisha tutakwenda mikoa yote inayolima miwa ili kusikiliza, kupokea changamoto na kuzitatua kwa pamoja. Tutahakikisha tunamaliza upungufu huu wa sukari hapa nchini, wawekezaji tuelezeni sisi serikali changamoto zinazowakabili wakati wa uzalishaji ili tukae na kuona njia bora ya utatuzi wake, kuacha mazingira bora ya uzalishaji”. Amesema Naibu Waziri Mgumba.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Prof. Kenneth Bengesi ambaye aliongozana na Naibu Mgumba amesema kwamba bado mahitaji ya sukari hapa nchini ni makubwa na kutoa wito kwa wawekezaji waliowekeza katika viwanda vya sukari kuitazama fursa hiyo na kuishughulikia.

“Tumeweka mazingira rafiki ya wawekezaji kuwekeza katika sekta ya sukari, tunawakaribisha kwa sasa, serikali imedhamiria kuingia katika uchumi wa kati wa viwanda”. Ameeleza Prof. Bengesi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter