Home VIWANDAMIUNDOMBINU Wananchi tunzeni miundombinu ya maji-DAWASA

Wananchi tunzeni miundombinu ya maji-DAWASA

0 comment 134 views

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange ametoa wito kwa wananchi kutunza miradi na miundombinu ya maji ili iweze kuwahudumia na hivyo kuondokana na tatizo la ukosefu wa maji.

“Niwaombe wananchi watunze miundombinu ya maji maana ujenzi wake ni gharama sana tofauti na wao wanavyofikiria wanapoona maji yamewafikia majumbani”. Amesema Jenerali Mstaafu Mwamunyange.

Katika ziara ya wajumbe wa bodi hiyo kutembelea miradi mbalimbali ya DAWASA,  Jenerali Mwamunyage ametembelea ujenzi wa mradi wa bomba la maji kutoka Kibamba hadi Kisarawe utakaozalisha Lita Milioni 4 za maji kwa siku na wananchi mbalimbali wa maeneo ya Kisarawe watafaidika na maji. Mwenyekiti huyo ameeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa tenki hilo na kusema endapo wakandarasi wataendelea na kasi hiyo, ujenzi huo utakuwa umekamilika hadi kufikia Septemba.

Mbali na hayo, Jenerali Mstaafu Mwamunyange ametembelea tenki la maji lenye ukubwa wa lita milioni 10 kwenye eneo la Kibamba na kuoneshwa pampu nne za kusukumia maji hadi Kisarawe.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter