Home BIASHARA Ufafanuzi bei holela ya mikate Zanzibar

Ufafanuzi bei holela ya mikate Zanzibar

0 comment 119 views

Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar, Hassan Mohamed Hafidh amesema serikali ya mapinduzi visiwani humo inatekeleza sera ya biashara huria hivyo haiwezi kupanga bei ya bidhaa zinazozalishwa ndani hasa zile za bidhaa za vyakula kama mikate. Naibu Waziri Hafidh amesema hayo wakati akitoa majibu kwa mwakilishi aliyehoji kwanini serikali haiingilii kati suala hilo kutokana na bei ya mikate kupanda kiholela.

Bei ya bidhaa ya mkate imekuwa ikiongezwa bila mpangilio na wafanyabiashara wa bidhaa hiyo, hali ambayo imekuwa ikileta kero kwa wananchi ambao wamekuwa wakitaka kufahamu kama serikali inaweza kuingilia kati suala hilo na kulitafutia suluhisho.

“Serikali haipo tayari kuingilia kati masuala ya bei ya bidhaa zinazotengenezwa nchini ikiwemo mikate ya boflo lakini sisi tunachosisitiza zaidi ni ubora” Amesema Naibu huyo.

Aidha, Naibu Waziri Hafidh amesema Pemba inatengeneza mikate ya boflo inayoridhisha ubora wake, tofauti na ile ya Unguja ambayo bado ubora wake sio wa hali ya juu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter