Home VIWANDAMIUNDOMBINU Barabara zijengwe kwa viwango-Jafo

Barabara zijengwe kwa viwango-Jafo

0 comment 121 views

Baada ya kukamilika kwa maabara za kisasa za kupima udongo na maligahfi katika wilaya tatu za jijini Dar es salaam kupitia Mradi wa Uboreshaji wa jiji la Dar es salaam (DMDP) ulio chini wa Benki ya Dunia (WB), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amezitaka halmashauri zote kuhakikisha barabara zinazojengwa ni za viwango vya hali ya juu.

Jafo amesema hayo wakati wa uzinduzi wa maabara hiyo Kinondoni akiwa na wawakilishi kutoka WB ambao wametoa takribani Sh. 660 kufadhili miradi ya DMDP. Waziri huyo ameeleza kuwa, kuwepo kwa maabara hizo kutasaidia zoezi la upimaji udongo unaotumika kujenga barabara ili kuepuka kujenga zile ambazo hazina ubora.

“Kutokana na maabara hii, sitaki kuona barabara zikijengwa chini ya kiwango, ninachotaka miradi ya DMDP ya barabara idumu kwa miaka 20 sio miwili kwa kuwa sitarajii kuona zikiwa na mashimo mashimo. Kama maabara ipo na malighafi zinazoenda kujengewa barabara hazina ubora watawajibika na  hatua zitachukuliwa dhidi yao”. Amesema Waziri Jafo.

Naye Sameh Wahba, Mwakilishi wa Benki ya Dunia amesema benki hiyo itaendelea kushirikiana na serikali kwani wameridhishwa na maendeleo ya miradi inayotekelezwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter