Home BIASHARA Vikwazo biashara vyatajwa

Vikwazo biashara vyatajwa

0 comment 134 views

Japokuwa serikali imefanya jitihada za kufuta tozo mbalimbali ili kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Maendeleo ya Sekta binafsi na Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu, Christopher Mramba, ametaja vikwazo vikuu katika sekta ya biashara kuwa ni kodi za kupita kiasi, leseni, vibali na ada.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wizara, taasisi za serikali na sekta binafsi wakishirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi  na Kijamii  (ESRF) wameandaa mpango wa miaka mitatu ambao unategemea kuanza mwaka wa fedha 2018/19 hadi 2020/21 ili kutatua changamoto hizo.

Hata hivyo Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, na Uwekezaji, Dorothy Mwaluko amesisitiza kuwa changamoto hizo lazima zifanyiwe kazi na kwamba ni wakati muafaka wa serikali kufanya vitu kwa uhalisia ili kupata maendeleo.

“Usije ukafurahia umeweka malengo ya kutufurahisha wakati kiuhalisia hilo lengo hutokaa utimize, jiangalie sana katika nyumba yako una uwezo kutekeleza kitu gani kwa uhalisia, tusipende kukuza mambo wakati hatuna uwezo,tuende mdogo mdogo safari ni ndefu”. Amesema Katibu huyo.

Aidha, ameongeza kuwa kupitia maboresho yatakayofanyika serikali itaongeza mapato ya kodi kwani wafanyabiashara watapata maendeleo katika biashara zao na kuondokana na umaskini hivyo pato la taifa kuongezeka.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter