Home FEDHA Acacia yapewa siku 7 kulipa fidia

Acacia yapewa siku 7 kulipa fidia

0 comment 100 views

Serikali imeagiza mgodi wa Acacia North Mara kuwalipa fidia stahiki wananchi wanaodai mgodi huo ndani ya siku saba. Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema hayo baada ya wananchi 203 kutoka vijiji vinne vinavyozunguka mgodi huo kutoa kilio chao wakidai kuwa mgodi huo uliwaandikia hundi yenye viwango vidogo hali iliyowafanya wagome kupokea fedha hizo licha ya kufanyiwa tathmini tangu mwaka 2014.

“Ninawapa siku saba kuanzia leo kufanya uhakiki na ifikapo Machi 30 mwaka huu muwe mmeshawalipa fidia wananchi hawa wanaodai fidia za mali zao ili kuondoa malalamiko”. Amesema Biteko.

Neema Daudi ni mmoja wa wananchi walioandikiwa fidia ya kiwango cha chini ambapo alikuwa na nyumba mbili na ardhi ya shamba aliandikiwa hundi ya Sh. 41,159 huku Dickson Ryoba wa kijiji cha Nyabichune amedai kuandikiwa hundi ya Sh. 41,449 ambayo hailingani na mali zake.

Mbali na hayo, Waziri Biteko, amewataka Acacia kukarabati mabwawa yao ya maji machafu kwani yanapotiririsha maji hayo kwenye mito iliyopo karibu na makazi ya wananchi maji hayo yanahatarisha afya zao.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter