Home WANAWAKE NA MAENDELEO Balozi Donnell: Wanawake washirikishwe zaidi kiuchumi

Balozi Donnell: Wanawake washirikishwe zaidi kiuchumi

0 comment 101 views

Balozi wa Canada hapa nchini, Pamela Donnell amezitaka taasisi binafsi kuongeza ushiriki wa wanawake katika sekta mbalimbali za kiuchumi. Donnell amesema hayo wakati wa maadhimisho ya nane ya jukwaa la Canada na Tanzania na kuongeza kuwa, uwepo wa wanawake katika shughuli za kiuchumi huchochea uzalishaji na usawa.

Ameeleza kuwa, kampuni binafsi zitafaidika pale zitakapofungua milango zaidi ya ajira kwa wanawake na kuwapatia nafasi za kuwa viongozi kwani hata takwimu zinaonyesha kuwa kampuni ambazo zina idadi kubwa ya wanawake katika nafasi za uongozi zinazalisha kuliko zile zenye uwakilishi mdogo.

“Kampuni zenye kiwango kikubwa cha usawa wa kijinsia katika nguvu kazi yao na uongozi wa juu, huvuna faida nyingi”. Amesema Balozi huyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), John Mnali amesema taasisi hiyo inafahamu changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wanawake katika sekta binafsi na kuongeza kuwa, Tanzania na Canada zinaendelea kushirikiana ili kuvutia wawekezaji kutoka nje ya nchi na kufanikisha azma ya Tanzania kufikia uchumi wa viwanda.

“Tanzania na Canada wamekuwa marafiki wazuri na ninaelewa kuwa serikali ya Canada inaisaidia Tanzania katika kupunguza umaskini kwa kuzingatia mahitaji ya binadamu hasa wanawake na watoto. Wanawake ndio wazalishaji wakubwa katika familia nyingi. Wanawake wa Tanzania wanapaswa kupewa uwezo na usawa katika kutawala uchumi”. Amesema Mnali.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter