Home BIASHARAUWEKEZAJI Syria yavutiwa uwekezaji Tanzania

Syria yavutiwa uwekezaji Tanzania

0 comment 175 views

Ofisa Uhamasishaji Uwekezaji wa Mamlaka ya Ukanda Maalum ya Uwekezaji (EPZA), Grace Lemunge amesema maonyesho ya kimataifa ya Syria yanayoendelea jijini Dar es salaam yamepelekea wawakilishi kadhaa kutoka nchi hiyo kuvutiwa kuwekeza nchini hasa katika sekta ya viwanda.

“Wawakilishi wa kampuni zinazoshiriki katika maonyesho ya kimataifa ya Syria waliotembelea banda la EPZA, wamevutiwa sana na fursa za uwekezaji hasa kwenye viwanda kwa kupitia mamlaka ya EPZA”. Amesema Lemunge.

Pamoja na hayo, Ofisa huyo pia ameeleza kuwa kupitia EPZA, muwekezaji ana uwezo wa kuwekeza katika maeneo ya ukanda maalumu (SEZ) ambapo asilimia 80 za bidhaa zitakazozalishwa huuzwa nje ya nchi na zile zitakazosalia huuzwahapa  nchini.

Kwa upande wake, Ofisa Mwandamizi wa Uhamasishaji EPZA, Panduka Yonazi amesema maonyesho hayo yamewanufaisha wadau mbalimbali wa uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi hasa kupitia elimu wanayoipata kuhusu uwekezaji pamoja na fursa mbalimbali.

“Wafanyabiashara wazawa ambao wanashiriki katika maonyesho ya kimataifa ya Syria wamekuja kwa wingi sana katika banda la EPZA ili kupata taarifa juu ya fursa ya uwekezaji katika viwanda nchini”. Ameeleza Yonazi.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter