Home BIASHARA Wabunge walalamikiwa tozo kubwa mifugo

Wabunge walalamikiwa tozo kubwa mifugo

0 comment 131 views

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa mifugo kutoka Tanzania kwenda Kenya kutoka Halmashauri ya Longido, Saruni Laizer amewasilisha malalamiko kuhusu tozo kubwa za ushuru wanazotozwa wafanyabiashara hao kwa Naibu Waziri wa Mifugo, Abdallah Ulega na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji pamoja na Katibu Mkuu wake, Prof. Elisante Ole Gabriel.

Wafanyabiashara hao wameeleza kuwa tozo zinazotozwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa sasa zinaanzia Sh. 15,00 hadi Sh. 30,000 kwa ng’ombe mmoja na Sh. 4,500 hadi 7,500 kwa mbuzi jambo ambalo linawakwamisha wafanyabiashara hao. Mwenyekiti huyo amesema kwamba kabla Wizara haijachukua mnada kutoka Halmashauri ya Longido, wafanyanyabiashara walikuwa wakiingiza magari 25 ya ng’ombe na magari 30 ya mbuzi lakini biashara hiyo imezorota mbapo sasa gari 1 la ng’ombe na manne ya mbuzi huingia mnadani hapo.

“Mh. Naibu Waziri tuliwahi kulalamika juu ya tozo hizi kuwa ni kubwa na kwamba siyo rafiki kwa wafanyabiashara leo (jana) leo mbele ya Kamati hii wabunge nataka niwaambie kuwa kiatu kinatubana na kinakaribia kuleta kidonda cha kukamua usaa. Naomba nikutahadharishe kuwa ni vyema ukatununulia kiatu kipya, kuliko kutumia gharama kubwa kuja kutibu kidonda”. Amesema.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa amesema kuwa Wizara hiyo inatakiwa kufanya marekebisho ya kanuni hizo kabla ya kuanza kwa bunge la bajeti. Aidha, Kamati hiyo imepinga Halmashauri kupata ushuru wa Sh. 1,000 kwa ng’ombe na Wizara kupata 4,000 na Sh. 500 kwa mbuzi mmoja na wizara kupata Sh. 1,000 na kutaka mapato yagawanywe nusu kwa nusu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter