Home BIASHARA Chumvi ya Lindi yatamba sokoni

Chumvi ya Lindi yatamba sokoni

0 comment 270 views

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Lindi, Jomaary Satura amesema bidhaa ya chumvi inashika nafasi ya nne katika kuingiza mapato mkoani humo kutokana na ubora wake ambao umepelekea kupata soko kubwa katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Satura amesema hivi sasa bidhaa hiyo inauzwa nchi za Rwanda, Burundi na Congo na kwamba uzalishaji wake unazingatia ubora. Pamoja na nchi hizo, pia ametaja mikoa ambayo imekuwa ikinunua chumvi hiyo kuwa ni Dar es salaam, Pwani, mikoa ya nyanda za juu kusini kama Ruvuma, Mbeya, Iringa na Njombe.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa upande wa Lindi una mashamba ya chumvi 144 na sehemu kubwa ya chumvi huzalishwa katika kiwanda cha Neel Salt kilichopo Mkuranga mkoani Pwani. Aidha, Mkurugenzi wa kampuni ya Mshindo Salt, Said Ali Tamimy amesema kuwa anafuata taratibu na Sheria za uzalishaji wa chumvi, na kwamba uzalishaji katika kampuni yake umeongezeka baada ya kununua mashine ya kusaga chumvi.

Tamimy ameeleza kuwa katika kila shamba kuna mabirika 20 ambayo huzalisha viroba 30,000 vya kilo hamsini. Ameongeza kuwa anategemea siku za mbeleni kuzidi kukuza soko kwa kuuza nchini Uganda na Congo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter