Home FEDHA Bajeti izingatie idadi ya watu- RC Mahmoud

Bajeti izingatie idadi ya watu- RC Mahmoud

0 comment 127 views

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud ametoa wito kwa Kamati ya Kilimo, Biashara na Fedha ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuzingatia idadi ya wakazi kila mkoa wakati wa mgawanyo wa bajeti ya fedha kwa serikali za mitaa. Mahmoud amesema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo na kuongeza kuwa kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, Mjini Magharibi ina takribani watu 597,000 (Sawa na asilimia 49 ya watu wote Zanzibar) huku akipendekeza angalau asilimia 48 ya bajeti ielekezwe kwenye mkoa huo.

Pamoja na hayo, amewataka wajumbe hao kuzingatia suala ya miundombinu hususani barabara kwani zilizokuwepo ni chakavu. Kuhusu sekta ya kilimo na ufugaji, Mkuu huyo amesema serikali imeanza kuweka msisitizo kwa kuunda vikundi vya ushirika vya vijana maalum kwa ajili ya ufugaji ili kukuza ajira.

“Hivi karibuni mimi mwenyewe nikiambatana na viongozi wa Mabaraza ya Manispaa tulifanya ziara maalum Tanzania Bara ili kujifunza namna watakavyoweza kuimarisha sekta ya ufugaji kwa mkoa Mjini Magharibi ikiwa ni mikakati ya kuwasaidia vijana”. Amesema Mahmoud.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mwinyihaji Makame amesema lengo la ziara hiyo ni kufuatilia utekelezaji wa ahadi za mawaziri katika bajeti zao. Makame amesema wajumbe hao pia walipata nafasi ya kuangalia maendeleo ya miradi na kujionea mafanikio na changamoto zilizopo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter