Home BIASHARA Masoko mawili ya madini kujengwa Simanjiro

Masoko mawili ya madini kujengwa Simanjiro

0 comment 141 views

Ofisa Madini Mkazi wa mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima amesema katika utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli, mkoa huo umejipanga kujenga masoko mawili ya madini, miji midogo ya Mirerani na Orkesumet. Ntalima ameeleza kuwa japokuwa serikali imeagiza kila mkoa kuwa na soko moja la madini, kutokana na jiografia, mkoa huo unapaswa kuwa na masoko angalau mawili kwa sababu ya umbali wa kilomita 120 kutoka Mirerani hadi Orkesumet.

“Wafanyabiashara wa madini ya vito vya rubi, green na mengine watatumia soko hilo la Orkesumet na kurahisisha uuzaji wa madini katika mkoa wetu wa kimadini wa Simanjiro. Wafanyabiashara wa madini ya green na Landanai na Lemshuku watajiamulia wenyewe kuuza popote watakapopenda watakapoona ni karibu kati ya Mirerani na Orkesumet”. Amefafanua Ofisa huyo.

Baadhi ya wafanyabiashara wa madini katika mkoa huo wamesema ujenzi wa masoko hayo utaimarisha uchumi kwa kiasi kikubwa.

“Kuwapo masoko hayo ni hatua nzuri kwani kila mtu ataamua mwenyewe kutumia soko atakaloona lipo karibu kati ya Mirerani na Orkasumet”. Amesema mfanyabiashara mmoja.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter