Home BIASHARAUWEKEZAJI Watendaji kikwazo sekta ya uwekezaji- Magufuli

Watendaji kikwazo sekta ya uwekezaji- Magufuli

0 comment 121 views

Rais John Pombe Magufuli amewataka watendaji wa serikali kubadilika na kuwachukulia wawekezaji kama marafiki zao na sio maadui. Rais Magufuli amesema hayo wakati akizindua kiwanda cha majani ya chai kijiji cha Kabambe mkoani Njombe.

“Kuna matatizo ya uwekezaji katika nchi yetu, saa nyingine inakuwa inakatisha tamaa kuja kuwekeza. Mtu anapotaja kuja kuwekeza saa nyingine anapata shida, masharti ni ya ajabu, baadhi ya watendaji wetu wamekuwa ni matatizo katika uwekezaji. Ninawaomba watendaji ndani ya serikali wabadilike, mtu anataka kuja kujenga kiwanda unamzungusha mpaka mwaka mzima. Yeye ana pesa zake anataka kujenga kiwanda hata mabati na ajira zitapatikana hapa, lakini watu wamekuwa na vichwa vigumu sana, nafuu vichwa vya kamongo. Hawataki kuelewa wapo wawekezaji wamekuja hapa wamewekewa mikwara mpaka wakaamua kwenda nchi za jirani”. Amesema Rais Magufuli.

Pamoja na hayo, ameongeza kuwa masharti yasiyokuwa na mantiki na rushwa ni kati ya mambo yanayokwamisha sekta ya uwekezaji kwani nchi ina fursa nyingi, na kwamba wahusika waliopo katika sekta hiyo ndio tatizo.

“TIC (Kituo cha Uwekezaji Tanzania) ilikuwa Wizara ya Viwanda na Biashara niliona mambo hayaendi vizuri sasa nimeamua kuirudisha Ofisi ya Waziri Mkuu, nikiona mambo hayaendi nitairudisha kwangu”. Amesema Rais Magufuli.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter