Home FEDHA Serikali yatenga mabilioni kulipa fidia

Serikali yatenga mabilioni kulipa fidia

0 comment 96 views

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ameeleza kuwa serikali ina mpango wa kutumia Shilingi Bilioni 21.6 katika mwaka wa fedha 2019/2020 kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi wa maeneo ya Kisarawe, Kibaha (Mjini na Vijijini), Chalinze na Kiluvya. Naibu Waziri Mgalu amesema hayo bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Sylvester Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu wakati serikali inaendelea kukamilisha taratibu za malipo hayo.

Pia ameeleza kuwa, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linatekeleza mradi huo mkubwa wa umeme wa msongo wa KVA 400 Kinyerezi kupitia mikoa ya Pwani, Morogoro, Singida na Arusha ili kuongeza upatikanaji wa umeme katika maeneo ya ukanda wa kaskazini na mashariki.

“Serikali kupitia TANESCO Januari 2019 ilitangaza zabuni kumpata mtaalamu mshauri kufanya upembuzi yakinifu ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Rufiji hadi Chalinze na kuhuisha upembuzi yakinifu wa njia ya umeme wa msongo kilovoti 400 Kinyerezi-Chalinze”. Amefafanua Naibu Mgalu.

Kuhusu fidia kwa wananchi wa Mkuranga, Kibiti na Kilwa Mgalu amesema serikali itakutana na TANESCO ili kujua watamaliza lini malipo ya fidia hiyo. Hadi sasa, shirika hilo limeshalipa Bilioni 30 kati ya Bilioni 50 ambazo walikuwa wanatakiwa kuwalipa wananchi hao.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter