Home BIASHARA Vodacom yawadatisha wateja wake na data

Vodacom yawadatisha wateja wake na data

0 comment 86 views

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc, leo imezindua kampeni kabambe ya data iitwayo “Data Datani’ ambayo inawezesha wateja wake kupata bonus Mb hadi mara mbili zaidi kila wanunuapo bando la intaneti. Kampeni hiyo imezinduliwa katika viwanja vya Mbagala Zackhem jijini Dar es Salaam.

Kampeni ya Data datani inalenga kuwawezesha watumiaji wa intanet kufaidi zaidi matumizi ya vifurushi vyao na pia kuwajuza mbinu mbali mbali za kutunza data isiishe kwa haraka, jambo ambalo limekuwa likiwatatiza wateja wake kwa muda mrefu.

Ili kupata ofa hii, wateja wa Vodacom Tanzania Plc wanatakiwa kupiga *149*01# kisha chagua intaneti, halafu chagua intaneti bando kisha nunua kifurushi, hii itakuwezesha kupata hadi mara mbili ya bando uliyonunua awali kwa bei ile ile.

Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa (Mbele) akizungumza na wananchi wakati wa uzindunzuzi wa kampeni ya Data Datani iliyofanyika viwanja vya Mbagala Zackiem hapo jana. Data Datani ni huduma inayowezesha wateja wa Vodacom kupata Mb hadi mara mbili zaidi ya kiwango walichonunua kila wanunuapo bando la intaneti.

Katika Uzinduzi wa kampeni hiyo kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa alitilia mkazo umuhimu wa data katika maisha ya kila siku. “Tukiwa ni Kampuni inayoongoza nchini kwa kutoa intaneti yenye kasi zaidi nchini, ni muhimu kuzingatia pande zote mbili za sarafu, yaani huduma na wateja wetu. Ndio maana tumeleta kampeni hii ili kuwawezesha wateja wetu kupata zaidi ya kile walicholipia kila wanaponunua bando la data,” alisema Linda huku akiongeza kwamba wanafahamu umuhimu wa data hasa katika zama hizi za kidijitali, habari zote na biashara ziko mitandaoni, hivyo wasingependa ukosefu wa data uwe kikwazo kwa wateja wao katika kufanikisha shughuli zao za kila siku.

Mwaka 2017 Kampuni ya Vodacom Tanzania ilizindua mtandao wa 4G katika mkoa wa Dar es Salaam ili kuwawezesha wateja wake kupata intaneti yenye kasi zaidi, na mpaka sasa mtandao huu wa 4G umesambaa kufikia mikoa 24.

Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa (wapili kulia) pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifurahia uzinduzi wa kampeni ya Data Datani, iliyofanyika viwanja vya Mbagala Zackiem hapo jana. Data Datani ni huduma inayowezesha wateja wa Vodacom kupata Mb hadi mara mbili zaidi ya kiwango walichonunua kila wanunuapo bando la intaneti.

Mfanyabiashara na mkaazi wa Mbagala bwana ………. aliyehudhuria uzinduzi huu nae alisema, “Sasa ni wakati wa kudata datani, internet sio tu teknolojia bali pia ni kiuwezeshaji. Inatuwezesha kupata habari haraka, inatuwezesha kufanya biashara za mtandaoni, inawezesha serikali kupata kipato na kuwezesha shughuli za kijamii, yani kudata, ni zaidi ya data tu”.

Kampeni hii inalenga kuwezesha wateja kutumia data zaidi na kikamilifu kwa shughuli zao zote za mtandaoni bila kuwa na wasiwasi wa data kuisha.

Ili mteja aweze kufurahia huduma hii anapaswa kununua kifurushi kupitia mfumo wowote iwe ni M-Pesa, vocha, My Voda App, na ataweza kuperuzi habari, kuangalia video, kusikiliza muziki au kununua bidhaa mtandaoni. Changamkia fursa hii kwa kubofya *149*01, pata kifurushi chako cha intaneti uendelee kudata datani.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter