Home BIASHARAUWEKEZAJI Kampuni zachangamkia uwekezaji Iringa

Kampuni zachangamkia uwekezaji Iringa

0 comment 133 views

Baada ya mkoa wa Iringa kuita wawekezaji ili kunusuru wakulima wa chai, kampuni tatu za DI Group (Kenya), Rwandan Mountain Tea Limited (Rwanda) na E-Vision Consulting ya Tanzania zimedhamiria kuwekeza kwenye viwanda vya usindikaji chai wilayani Kilolo mkoani humo. Hayo yamebainishwa wakati wa mkutano uliowakutanisha wawekezaji hao na uongozi wa mkoa ikiwa ni jitihada mojawapo ya serikali kufufua kiwanda ambacho kimesitisha uzalishaji wa zao hilo kwa takribani miaka 15 na kupelekea hasara kubwa.

Katibu Tawala mkoani humo, Happiness Seneda ametoa shukrani kwa wawekezaji hao na kusema hatua hiyo ni ishara kwamba wanalenga kuwainua wakulima wa Kilolo. Wakati huo huo, Mkuu wa mkoa wa Iringa, Ally Hapi amesema kuna mazingira rafiki ya utendaji kazi katika maeneo ambayo wawekezaji hao wamepanga kuwekeza ikiwemo maji, umeme wa uhakika pamoja na barabara.

“Niwahakikishie kwamba haya mliyoyasema ya barabara yatakwenda kufanyika hivi sasa tunavyozungumza Mkandarasi yupo barabarani kilometa 32 Iringa-Kilolo inafanyiwa kazi na tumeamua kufanya kwa wazi ili wawekezaji wasishindwe kufanya uwekezaji”. Amesema Mkuu huyo wa Iringa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya DI Group, Dk. David Langat amesisitiza kuwa wamejipanga kufanya kazi na kushukuru uongozi mzima wa mkoa huo pamoja na serikali kwa ujumla kwa kuwapa uhakika wa miundombinu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter