Home VIWANDAMIUNDOMBINU Kamwelwe aagiza tozo kufutwa

Kamwelwe aagiza tozo kufutwa

0 comment 97 views

Kufuatia uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) uliofanyika Jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe ameitaka Bodi hiyo kufuta tozo za usafirishaji mizigo bandarini zisizokuwa za kisheria ndani ya mwezi mmoja ili kuwezesha ushindani wa kibiashara.

Waziri Kamwelwe ameitaka Bodi hiyo kufanya kazi kwa juhudi ikiwa ni pamoja na kupitia na kujiridhisha na tozo zinazotozwa katika bandari hiyo, lengo likiwa ni kusaidia bandari kuchangia uchumi na maendeleo ya taifa.

“Wakati huu ninapoizindua Bodi hii naomba mkahakikishe mnaenda kufanya kazi kwa juhudi, lakini kubwa ni kuziondoa tozo zote mzigo zisizo na manufaa na hili mkalisimamie kikamilifu mkishindwa baada ya siku thelathini nitaita vyombo vya habari na kutangaza kuzifuta”. Amesisitiza Kamwelwe.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Tadeo Satta ametoa shukurani kwa Rais Magufuli kwa uteuzi huo na kuahidi kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo ya serikali. Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA),Deusdedit Kakoko amesema uzinduzi huo utasaidia TPA kutimiza malengo yake kwa sababu kutokuwepo kwa chombo hicho kwa muda mrefu kumeleta udhaifu katika baadhi ya shughuli bandarini.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter