Home AJIRA Stahiki zipi ni muhimu kwa wafanyakazi wako?

Stahiki zipi ni muhimu kwa wafanyakazi wako?

0 comment 114 views

Faida mbalimbali kwa wafanyakazi zinaendelea kuwa muhimu sana katika mambo ambayo wafanyakazi hufikiria wakati wanachukua au kuamua kukaa na kazi. Lakini chini ya nusu ya biashara ndogondogo kwa sasa wanatoa faida kwa mfanyakazi, kulingana na utafiti uliofanywa na Clutch. Je, huitendei haki biashara yako kwa kutotoa faida ambazo timu yako wanataka? Basi unatakiwa kujua haya.

Faida za mfanyakazi zilizo zoeleka

Mara nyingi biashara ndogo ndogo hutoa faida hizi kwa wafanyakazi wao:

Bima ya afya : 69%

Mipango mingine ya kustaafu : 52%

Likizo ya familia : 48%

Malipo wakati wa likizo (PTO) : 45%

Biashara inavyokua, na faida kwa wafanyakazi huongezeka. Karibia asilimia sabini (68%) ya makampuni yenye wafanyakazi 11 hadi 50 hutoa faida kwa wafanyakazi na 76%ya wale walio na wafanyakazi zaidi ya 50 pia hutoa, ikilinganishwa na 32% ya wale wenye wafanyakazi wawili hadi kumi.

Makampuni makubwa huwa na fedha zaidi za kutumia kwenye faida; kwa kuongeza, ikiwa kampuni ina wafanyakazi 50 au zaidi, kwa ujumla huwa inakuwa chini ya Affordable Care Act (ACA) na Family Medical Leave Act (FMLA). ACA inamuamuru muajiri kutoa bima ya afya kwa wafanyakazi au kulipa penati wakati FMLA inawataka waajiri kutoa malipo ya familia na matibabu kwa wafanyakazi wenye vigezo.

Wafanyakazi wanataka faida gani?

Bima ya afya na mipango ya kustaafu ni faida maarufu kwa wafanyakazi. Hata hivyo, eneo moja ambalo biashara ndogondogo wanashindwa kuwatekelezea wafanyakazi ni malipo wakati wafanyakazi hawapo kazini (timeoff).

Chini ya nusu (45%) ya makampuni madogo ambayo hutoa faida kutoa PTO. Miongoni mwa wale ambao hutoa PTO, 5% tu hutoa siku chache zaidi katika siku tano za biashara za PTO, kuonyesha kwamba biashara ndogo ndogo zinaelewa umuhimu wa kuwapa likizo wafanyakazi.

Lakini bado njia ni ndefu. Uchunguzi tofauti uliofanywa na MetLife unaelezea kuwa wakati wa likizo usio na ukomo ni “faida inayojitokeza” wafanyakazi wanaelezea maslahi mengi. Haishangazi kuwa kutoka kwa biashara ndogo zilizofanyiwa uchunguzi na Clutch asilimia 19 ya wale wanaoongeza faida mpya mwaka huu wanafikiria kuongeza PTO.

Maboresho zaidi katika faida za wafanyakazi ni jambo zuri zaid kwa wafanyakazi wako. Wafanyakazi 93% katika utafiti wa MetLife wamesema uwezo wakuboresha faida zao ni kuweka chaguo la lazima-kuwa nayo au ni vizuri-kuwa nayo; karibia ¾ (72%)  wamesema kuwa na faida zilizoboreshwa kunawafanya wawe waaminifu zaidi kwa waajiri wao.

Kwa biashara ndogo, njia moja wapo ya kuboresha faida za wafanyakazi ni kwa kuwafanya wafanyakazi wapige kura kuhusu mambo wanayohitaji zaidi. Kwa mfano, 17% ya biashara ndogo alizofanyia utafiti Clutch kwa sasa zinalipa mikopo ya wanafunzi, na asilimia 8 wanafikiria kuiongeza mwaka huu.

Kuwasikiliza wafanyakazi

Maoni ya waajiriwa yana athari katika ofa ya faida za mfanyakazi katika biashara ndogo anaripoti Clutch. Karibu theluthi moja ya wafanyabiashara wadogo ambao hupanga kutoa faida mpya mwaka 2019 wanasema wanafanya hivyo kutokana na maombi ya mfanyakazi, na 27% wanaongeza faida ili wafanyakazi wasiwageuke. Ni wazi, wamiliki wa biashara ndogo wametambua kwamba makampuni mengi yanavyotoa manufaa mbalimbali basi wanatakiwa kwenda sawa na makampuni hayo ili wasipoteze wafanyakazi wenye thamani.

Licha ya biashara ndogo kuwa katika upande wa hasara linapokuja suala la kutoa faida (malupulupu) kwa mfanyakazi, karibia 1/3 ya biashara (30%) hawana rasilimali kwa ajili ya Rasilimali watu (HR).

Katika makampuni madogo yenye kitengo cha rasilimali watu, karibu theluthi mbili ambayo ni 64% hutoa faida ya mfanyakazi. Na makampuni ambayo hayajajikita katika masuala ya rasilimali watu ni asilimia 10 tu ya makampuni hayo hutoa faida za mfanyakazi. Bila  aina fulani ya mpango rasmi wa programu ya Rasilimali watu (HR), inaweza kuwa vigumu kutekeleza, kuelimisha na kuwasaidia wafanyakazi katika faida zao.

Kumuajili Ofisa wa Rasilimali watu kufanya kazi moja kwa moja katika kampuni hakuwezi kuleta suluhisho la tatizo hili (Ingawa  asilimia 25 ya biashara ndogo kutokana na utafiti wa Clutch zimeajiri mtu wa HR), Unaweza pia kufanya kazi na mshauri wa mambo ya rasilimali watu (HR), kutumia shirika la wataalamu wa mambo ya waajiri (PEO), au kwenda nje ya rasilimali watu. Mbinu hizi hutumiwa kwa 9%, 8% na 6% na wamiliki wa biashara ndogo kwa mtiririko huo.

Faida mbalimbali wanazopewa wafanyakazi makazini imekuwa ni moja ya mambu muhimu kwa watu wanaotafuta kazi. Ikiwa unataka biashara yako ndogo iwavutie watu bora na wenye akili zaidi na kuwaweka katika hali ya furaha. Ni vizuri ukifikiria jinsi ya kuwapa ofa ya faida wanazotaka kama wafanyakazi.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter