Home BIASHARA Vodacom yazindua duka jipya jijini Tanga

Vodacom yazindua duka jipya jijini Tanga

0 comment 104 views

Kampuni ya simu ya Vodacom imezindua duka jipya jijini Tanga. Uzinduzi wa duka hilo ni miongoni mwa jitihada za Vodacom kurahisisha upatikanaji wa huduma za simu mikoani na kuwafikia zaidi wateja mikoa mbalimbali nchini.

Sherehe hiyo ya uzinduzi wa duka ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mh. Martin Shigela, Meneja wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen na Meneja wa Vodacom Mkoa wa Tanga, Fadhili Linga.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela (Kushoto) akisimkiliza Meneja wa Vodacom Mkoa wa Tanga, Fadhili Linga, (kulia) wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Vodacom jijini Tanga hivi karibuni. Aliyesimama katikati ni Meneja wa Vodacom Kanda ya kaskazini, Brigita Stephen. Uzinduzi wa duka hilo umelenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za simu katika mkoa ikiwa ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kuwafikia zaidi wateja wake katika mikoa mbalimbali nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Kampuni ya Vodacom jijini Tanga hivi karibuni. . Uzinduzi wa duka hilo  umelenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za simu katika mkoa ikiwa ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kuwafikia zaidi wateja katika mikoa mbalimbali nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mh. Martin Shigela (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa Meneja wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen (mkono wa kulia wa mkuu wa mkoa) wakati wa hafla ya uzinduzi wa duka jipya la Vodacom jijini Tanga hivi karibuni. Uzinduzi wa duka hilo ni miongoni umelenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za simu katika mkoa ikiwa ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kuwafikia zaidi wateja katika mikoa mbalimbali nchini. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Vodacom shop, Micheal Mtawali.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter