Home BIASHARA Vodacom yazindua duka jipya mkoani Kigoma

Vodacom yazindua duka jipya mkoani Kigoma

0 comment 121 views

Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom imezidi kupanua wigo wake kwa kuwafikishia wateja wake huduma za mawasiliano karibu zaidi.

Katika jitihada hizo Vodacom imezindua duka jipya mkoani Kigoma na sherehe hiyo kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenearali Mstaafu, Emmanuel Maganga na Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Ziwa, Domician Mkama.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga (kushoto) akisaidiwa kuweka alama ya kidole na Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Domician Mkama kwa ajili ya kusajili laini ya mtandao huo wakati wa hafla ya uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Kigoma mjini hivi karibuni.

Mkuu wa Mauzo wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Domician Mkama (kushoto) akizungungumza na wateja wa kampuni hiyo waliohudhuria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom lililopo kigoma mjini hivi karibuni. Kampuni ya Vodacom ina maduka takribani 100 na madawati ya huduma 350 (Service Desks) na inaendelea kupanua upatikanaji wa huduma ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kirahisi zaidi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga na wengine pichani ni watoa huduma wa duka hilo duka hilo jipya.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter