Home BIASHARA Wafanyabiashara wazuiwa soko la Sido

Wafanyabiashara wazuiwa soko la Sido

0 comment 104 views
Na Mwandishi wetu

Baada ya moto kuteketeza Soko la Sido jijini Mbeya siku chache zilizopita, wafanyabiashara wa soko hilo wameanza kujikusanya kwenye vikundi baada ya kukataliwa kuendelea na ujenzi wa mabanda ya kudumu ndani ya soko hilo.

Wakati hayo yakiendelea, shughuli za biashara katika masoko ya Mwanjelwa na Kabwe zimesimama huku maduka mengi yakiwa yamefungwa na wafanyabiashara hao kuhofia usalama wa mali zao.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Soko la Sido, Charles Syonga amesema kwa sasa wanasubiri maamuzi kutoka kwa bodi ya wajumbe wa soko hilo ndipo watatoa taarifa ya nini kifanyike kwa wafanyabiashara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga amesema polisi wamelazimika kuzuia wafanyabiashara baada ya agizo la serikali kukataza kufanya hivyo mpaka watakapopata kibali. Ameongeza kuwa polisi wanazuia misongamano ya watu ili kupisha kamati ya ulinzi na usalama iliyoundwa kuchunguza chanzo cha moto huo na hasara iliyopatikana.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter