Home BIASHARA Vodacom yashiriki kongamano la ‘Corporate Unwind’

Vodacom yashiriki kongamano la ‘Corporate Unwind’

0 comment 90 views

Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Vodacom imeshiriki kongamano la ‘Corporate Unwind’ lilioandaliwa na kampuni ya Smart Codes.

Kangamano hilo linalenga kuunganisha wadau mbalimbali katika sekta ya biashara na uvumbuzi ili kupata mawazo juu ya suluhisho za kidijitali kupitia teknolojia.

Vodacom imekua mstari wa mbele katika kutafuta suluhisho za kidijitali kwa kuvumbua teknolojia mbalimbali kutumia simu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi akieleza jambo kwa baadhi ya washiriki wa kongamano la Corporate Unwind lililoandaliwa na Smart Codes katika makao makuu yake jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Vodacom Tanzania ni kampuni ya mtandao wa simu inayoongoza Tanzania iliyojikita katika kuisaidia Tanzania kufikia uchumi wa kidigitali kwa kuvumbua mifumo suluhishi ya kidijitali kwa kutumia teknolojia ya simu. Kongamano hilo lilikutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya biashara na uvumbuzi pamoja na wafanyabiashara, taasisi na makampuni mashuhuri nchini Tanzania.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter