Kampuni ya gesi asilia ya Songas kwa mara nyingine imeshiriki kudhamini mashindano ya sayansi yajulikanayo kama ‘Young Scientist Tanzania’.
Mkurugenzi Mkuu wa Songas Nigel Whittaker alishiriki kuwapa medali na kombe wanafunzi mbalimbali walioibuka washindi katika nyanja ya ekolojia na baiolojia.
Songas imeshiriki mashindano haya kama jitihada za kuunga mkono juhudu za serikali katika kukuza sekta ya elimu nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Songas, Nigel Whittaker akikabidhi medali na kombe kwa Faudhia Juma Said na Zaina Yassin washindi wa kitengo cha Biolojia kutoka shule ya sekondari ya Mtwara Girls wakati wa maadhimisho ya mashindano ya sayansi yajulikanayo kama Young Scientist Tanzania, yaliyofanyika katika kumbi za JNICC, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Songas imekuwa moja kati ya wadhamini wa mashindano hayo kwa muda wa miaka nane sasa na hii ni katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha sekta ya elimu.