Home AJIRA Wasanii matajiri zaidi Tanzania

Wasanii matajiri zaidi Tanzania

0 comment 254 views

Tanzania imebahatika kuwa na wasanii wakubwa ambao wanaendelea kufanya vizuri na kuipeperusha vyema bendera yetu duniani kote. Leo hii, vijana wengi wamefanikiwa kupata ajira kutokana na muziki. Wasanii nao wamekuwa wakitumia nafasi zao kuinua vijana wengine katika jitihada za kupiga vita umaskini na kutengeneza ajira zaidi kupitia sanaa.

Hawa ni wasanii watano matajiri zaidi Tanzania ambao wameendelea kutufundisha kuwa kipaji chako kinaweza kuwa ajira yako kama utafanya kazi kwa bidii.

DIAMOND PLATNUMZ

Wengi tumemfahamu Naseeb Abdul Juma au maarufu zaidi kama Diamond Platnumz kupitia wimbo wa ‘Kamwambie’ ambao ulipokelewa vizuri na mashabiki. Diamond (29) hakutoka kwenye familia ya kitajiri lakini leo hii kwa mujibu wa jarida maarufu la Forbes, ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola za Marekani Milioni 5 na ndiye mwanamuziki tajiri zaidi nchini Tanzania.

Muziki wake umeendelea kupokelewa vizuri na mashabiki duniani kote na amefanikiwa kushirikiana na wasanii wakubwa kama Rick Ross, Ne-Yo, Omarion, Tiwa Savage, Fally Ipupa, Davido, Mr. Flavour, AKA, Morgan Heritage na Mafikizolo. Mbali na muziki, Chibu Dangote pia ameshirikiana na makampuni makubwa kama Pepsi, Vodacom na DSTV. Aidha, Platnumz ni Mkurugenzi wa WCB Wasafi na Wasafi Media (Wasafi TV na Wasafi Radio)

Diamond ni baba wa watoto watatu (Latiffah, Nillan na Dylan) huku mtoto wake wa nne akitarajiwa kuzaliwa hivi karibuni.

ALI KIBA

Bila shaka, huwezi kuzungumzia muziki wa Tanzania bila kumzungumzia Ali Kiba kwani yeye ni kati ya wasanii ambao wameendelea kuteka soko licha ya kwamba alianza muziki miaka ya 2000. Utajiri wa Ali K unakadiriwa kuwa Dola Milioni 4 za Marekani.

Baadhi ya nyimbo zake ni pamoja na Cinderella, Usiniseme, Nakshi Mrembo, Mwana na Aje. Mwaka 2015, Kiba alivunja rekodi ya Mkito,com kutokana na nyimbo zake kupakuliwa zaidi. Msanii huyu ana tuzo mbalimbali za kitaifa na kimataifa zikiwemo za Kilimanjaro Music Awards, BEFFTA Awards, MTV Europe Music Awards, Nafca, ASFA Awards pamoja na Soundcity Awards. Ali Kiba amepata nafasi ya kushirikiana na wasanii wakubwa kama Sauti Sol kutoka Kenya.

Mwaka 2016, King Kiba alisaini mkataba na kampuni maarufu ya muziki ya Sony na kuwa msanii wa pili barani Afrika nyuma ya Davido kusaini mkataba na kampuni hiyo.

PROFESSOR JAY

Mbunge huyu wa Mikumi alianza muziki miaka ya 1990, kipindi ambacho kulikuwa na changamoto nyingi katika sanaa. Baadhi ya nyimbo za Prof. J ni Nikusaidiaje (akimshirikisha Ferooz), Zali la Mentali (akimshirikisha Juma Nature), Hapo Sawa, Msinitenge, Yatapita (akimshirikisha Harmonize) na nyingine nyingi. Mbunge huyu ameendelea kuwekeza ipasavyo katika sanaa, ardhi/nyumba na usafiri/magari. Professor Jay anamiliki studio, nyumba na maduka kadhaa jijini Dar es salaam na Morogoro. Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali zikiwemo Venas News na Azania Post, utajiri wake unakadiriwa kuwa takribani Dola milioni 3.5 za Marekani.

LADY JAYDEE

Judith Wambura Mbibo au maarufu zaidi kama Lady Jaydee (miaka 40) naye yupo katika orodha ya wasanii matajiri hapa nchini. Jaydee ni msanii wa kwanza wa kike kufanya vizuri katika tasnia ya muziki. Komando amefanikiwa kutoa album saba; Machozi (2000), Binti (2003), Moto (2005), Shukrani (2007) Ya 5. The Best of Lady Jaydee (2012), Nothing But The Truth (2013) na Woman (2017). Inaelezwa kuwa gharama ya msanii huyo kufanya show moja sio chini ya $ 1,500.

AMBWENE YESSAYA ‘AY’

AY ni moja kati ya wasanii wakubwa na walioleta mageuzi katika tasnia ya muziki hapa nchini. Msanii huyu ambaye ni baba wa mtoto moja anamiliki kampuni ya Unity Entertainment ambayo inalenga kuwainua wasanii wachanga.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter