PESA TU ( Tovuti namba moja ya biashara)
PESA TU
Ni tovuti inayotoa nafasi kwa watu kupata taarifa kuhusu mambo mbalimbali ya uchumi ikiwemo biashara, viwanda, fedha na kilimo kutoka Tanzania na Afrika Mashariki. Pia utapata fursa yakujifunza kuhusu masuala ya ujasiriamali, hisa, uwekezaji na kilimo ufundi. Kupitia tovuti hii utaweza kuona matangazo mbalimbali ya ajira.
PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.
KUHUSU KAMPUNI
Website hii inamilikiwa na kampuni ya Mediapix Limited. MediaPix ni kampuni ya kimataifa inayohusika na musuala ya mawasiliano, matangazo na mahusiano ya umma katika bara la Afrika na Asia. Tunatoa huduma ya ushauri wa masoko kwa sekta binafsi, taasisi za serikali, asasi zisizo za kiserikali na mashirika ya kimataifa.Pia inahusika na usambazaji wa gazeti la kingereza la “The Exchange”linalotoka kila mwezi na linahusika zaidi na mambo ya uchumi katika nchi 5 za Afrika Mashariki.
WALENGWA
PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.
LENGO
Kuongeza uelewa na kufahamisha watanzania mambo mbalimbali ya uchumi na uwekezaji yanayoendelea Tanzania na nchi za jirani.
MATARAJIO
Kuwa tovuti ya mambo ya uchumi inayosomwa zaidi nakutumika kama chanzo cha habari kwenye vyombo vya habari vingine Tanzania.
MAKUSUDIO
- Kuwapatia wasomaji habari za uchumi zenye uhakika kutoka Tanzania na nchi za jirani kwa haraka punde zinapotokea.
- Kuongeza uwelewa kwa kutoa elimu ya maswala mbalimbali ya uchumi ikiwemo uwekezaji na hisa kwa watanzania.
- Kuwapatia taarifa watanzania kuhusu mwenendo na maendeleo ya uchumi wa nchi.