Home AJIRA Boti za uvuvi, vizimba kuinua wananchi kanda ya ziwa

Boti za uvuvi, vizimba kuinua wananchi kanda ya ziwa

0 comment 223 views

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua boti za uvuvi za kisasa 160 kwa wanufaika 989 pamoja na vizimba 222 vitakavyonufaisha watu 1,213.

Wanufaika hao ni wa mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Simiyu na Geita.

Akizungumza na wananchi Januari 30, 2024 katika uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza mara baada ya kuzindua na kukabidhi boti za uvuvi na vizimba vya kufugia samaki Rais Samia ameitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kushirikiana na Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri kudhibiti na kutokomeza vitendo vya uvuvi haramu.

“Serikali inafanya jitihada kuinua sekta ya uvuvi nchini kwa kuimarisha utendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili iendane na dhamira ya mageuzi yaliyokusidiwa,” amesema Rais Samia.

Ameitaka Wizara hiyo kuwachukulia hatua kali za kisheria wavuvi wanaokiuka taratibu za uvuvi salama.

“Serikali imejipanha kukuza sekta ya uvuvi kupitia miradi mbalimbali ikiwemo ununuzi wa meli za kisasa za uvuvi katika bahari kuu, ujenzi wa bandari za uvuvi katika maeneo ya Kilwa Masioko mkoani Lindi na Bagamoyo ili kuongeza pato la taifa,” ameeleza Rais.

Rais Samia amesema kundi kubwa la vijana na wanawake linaongoza kushiriki kwenye ajira zisizo rasmi hivyo serikali inarasimisha shughuli zao kwa kuwawezesha kupata zana na nyenzo za kisasa ili kujikimu kiuchumi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter