Benki ya CRDB imeongeza muda wa siku nne kwa wahitimu wapya wa vyuo vikuu kuomba nafasi za kazi.
Oktoba 22 benki hiyo ilitoa tangazo la nafasi za kazi “niajiri programu” katika fani mbalimbali kwa wahitimu wa vyuo vikuu wa mwaka 2019/2020 ambapo mwisho wa maombi ilikuwa Oktoba 31 lakini sasa muda umeongezwa hadi kufika November 4.
Tangazo lililotolewa na benki hiyo kupita ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram unaonesha fani hizo ni pamoja na Takwimu, Uhasibu, Masoko, Rasilimali watu, Afisa Habari na Usimamizi wa biashara.
CRDB imewataka wahitimu wenye umri usiozidi miaka 28 na ufaulu wa daraja la juu la pili kutuma maombi yao.
Bonyeza hapa kusoma zaidi.