Home AJIRA Mo Dewji kuongeza nafasi za ajira nchini

Mo Dewji kuongeza nafasi za ajira nchini

0 comment 147 views

Mfanyabiashara Mohammed Dewji amesema ana mpango wa kuongeza idadi ya wafanyakazi katika makampuni yake kutoka 32,000 mpaka 100,000 kufikia mwishoni mwa mwaka huu 2021.

Mo alisema lengo lake ni kushirikiana na serikali katika kujenga na kukuza uchumi wa nchi na wa mwananchi mmoja mmoja.

“Kwa sasa nimejikita kukuza ajira kwa kuongeza idadi ya wafanyakazi kutoka 32,000 hadi 100,000 kufikia mwisho wa mwaka,” alisema Mo.

Mo ambae alitajwa na jarida la Forbes kama tajiri namba 13 barani Afrika, alisema anavutiwa kwa kutambuliwa na jarida hilo jambo linalompa hamasa ya kuzidi kuwekeza katika maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla.

“Ninafanya kazi bega kwa bega na serikali ya rais Magufuli katika kuhakikisha sekta ya viwanda inafufuliwa nchini,” alieleza Mo.

Kwa mujibu wake, serikali imeongeza fursa za watu kuanzisha viwanda huku akibainisha kuwa lengo lake ni kuanzisha viwanda vitano hadi kumi kufikia mwishoni mwa mwaka 2021.

Dewji ambae ni Mkurugenzi wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL)  ametajwa kuwa na utajiri wa dola za Marekani bilioni 1.6

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter