Home AJIRA Unataka kuandika ‘Cover letter’ sahihi? soma hii

Unataka kuandika ‘Cover letter’ sahihi? soma hii

0 comment 402 views

Cover letter (barua ambatanishi) ni nyaraka ambayo huambatanishwa na CV ili kuweza kutoa maelezo zaidi kuhusu ujuzi na uzoefu wa muombaji wa ajira husika.

Watu wengi wamepata kazi za ndoto zao kutokana na uandishi mzuri wa barua ambatanishi. Sawa inaweza kuwa si jambo sahihi sana kuweka maelezo mengi sana katika barua moja lakini ni muhimu kujiweka katika nafasi ya mtu ambaye unatarajia akuajiri. Mara nyingi nafasi za kazi huombwa na watu wengi hivyo kupitia barua ambatanishi kila muombaji hupata nafasi ya kujieleza kwa muajiri kwanini achaguliwe yeye. Makosa katika barua ambatanishi yanaweza kumfanya muajiri afikirie kuwa haujali vya kutosha kuhusu ajira hiyo hivyo hata kama una vigezo barua hii inaweza kukufanya ukose kazi.

Hivyo ili kuandika barua ambatanishi kwa usahihi, ni muhimu kuzingatia haya:

  • Binafsisha barua yako, watu waliotangaza nafasi husika wanatakiwa kuona katika barua hii kuwa una shauku ya kufanya kazi katika kampuni yao. Hivyo fanya utafiti ili kujua historia fupi ya kampuni hiyo na watu wanaohusika ili kuweza kujua maelezo ya kuandika katika barua hii. Kwamfano, badala ya kuandika “Dear Sir/Madam” unaweza kuandika kwa ubinafsi kama “Dear Miss Paula Mrisho , COO”
  • Eleza tabia yako lakini kwa Utaalam, ni dhahiri kuwa katika CV(nyaraka ya udhahili) maelezo hutakiwa kuwa rasmi na ya kitaalam hiyo hupelekea mtu anayetaka kukuajiri asijue tabia na utu yako. ndio maana inashauriwa katika barua ambatanishi muhusika aeleze utu wake kwa umakini ili kumrahisishia muajiri kujua muhusika ni mtu wa namna gani na kama ataweza kumudu mazingira ya kazi hiyo. Hapa ni muhimu kuhakikisha maelezo hayazidi mipaka. Yale yote ambayo umeshindwa kuelezea katika CV katika barua hii ni mahali salama kwamfano kama uliacha shule miaka miwili na kuendelea unaweza kuelezea hapo na mengine mengi yanayohitaji maelezo zaidi.
  • Usisahau kujitambulisha, kwani mtu ambaye anataka kukuajili anaweza asiangalie CV yako na kuangalia moja kwa moja barua ambatanishi. Hivyo hakikisha utambulisho wako unavutia ili kumhamasisha muajiri kuweza kuendelea kujua uwezo na ujuzi wako

Hivyo basi, katika barua ambatanishi vipengele  vinavyotakiwa kuwepo ni kwa ufupi ni: Mawasiliano yako na anuani binafsi , Utambulisho- mfano “Dear Miss Paula Mrisho,COO” kisha eleza nafasi unayoomba na jinsi ulivofahamu kuhusu nafasi hiyo, na kumaliza kwa kuelezea elimu yako,ujuzi wako, malengo yako ya kazi ukilinganisha maelngo ya kampuni hiyo unakoomba kazi husika, kipengele kinachofuata unatakiwa kujieleza ili kuweza kumuhamasishaji kukupa kazi hiyo au la kwamfano eleza jinsi ujuzi wako na uzoefu utakavyoweza kunufaisha kampuni hiyo, na kipengele cha mwisho ni hitimisho ambapo unatakiwa kuwashukuru kwa muda wao na kuwajulisha kuwa ungependa kuitwa katika usahili.

Bonyeza linki hii kuona mfano wa barua ambatanishi https://www.livecareer.com/cover-letters/examples

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter