Home AJIRA Wafanyakazi wachekelea nyongeza mishahara

Wafanyakazi wachekelea nyongeza mishahara

0 comment 152 views

Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amerudisha nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi wa umma kwa kila mwaka iliyokuwa imeondolewa miaka saba iliyopita.

“Mambo ni moto, mambo ni fire” alisikika Rais Samia wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Dunia Meimosi mkoani Morogoro.

“Niseme pia, kuna nyongeza za mishahara za mwaka, ambazo kwa muda mrefu zilikuwa zimesitishwa, nikaona mwaka huu tuzirudishe, kwa hiyo wafanyakazi wote mwaka huu kuna nyongeza za mishahara na tunaanza mwaka huu na tutakwenda kila mwaka kama ilivyokuwa hapo zamani,” amesema Rais Dkt Samia.

Akizungumzia mambo yaliyotekelezwa na serikali yaliyotajwa katika maadhimisho ya Mei Mosi mwaka jana Rais Samia ametaja kulipwa mafao kwa wafanyakazi walioondolewa kazini kutokana na dosari katika vyeti vyao, kupunguza makato ya kodi ya PAYE kutoka 9% hadi 8%.

Nyingine ni mikataba ya hali bora za kazi kwa taasisi za umma, uundwaji wa mabaraza ya taasisis 40 ya umma ambazo haikuwa na mabaraza ya wafanyakazi, kulipwa mafao kwa wakati kwa wafanyakazi wanaostaafu, kuongezeka kwa mishahara.

“Lakini pia mlilalamikia na kuomba kuondoa tozo kwenye miamala ya kibenki, kuongezwa kwa umri wa mtoto wa mwananchama wa NHIF, kuongeza ajira, kupandisha madaraja ya watumishi na vilevile kulipwa stahili na nyongeza ya mishahara yao kama wanavyostahili.

Sasa nataka niseme kwamba mambo yote haya serikali imetekelza na naweza kusema kwa asilimia 95 wafanyakazi ninyi ni mashahidi, sehemu ndogo sana imebaki serikali inaendelea na utekelezaji,” amesema Rais Dkt Samia.

Rais Dkt Samia amesema serikali itaendelea kuboresha maslahi na maizngira ya kazi serikalini na sekta binafsi ili zipatikane ajira zenye usalama na staha kwa wote.

Kwa upande wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) imeitaka serikali kuondoa kodi kwenye marupurupu ikiwemo nauli za likizo na fedha zinazolipwa kwenye muda wa ziada.

Pia wameitaka serikali kuboresha kitengo cha Idara Kazi ili kupata ajira za staha.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni Mishahara Bora na Ajira za Staha ni Nguzo kwa Maendeleo ya Mfanyakazi, wakati ni sasa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter