Ni miaka mingine mitano tena kwa rais John Pombe Magufuli baada ya kutangazwa kushinda kiti cha urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 2020.
Mwanyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jaji Semistocles Kaijage alimtangaza rais Magufuli kuwa mshindi.
Kwa asilimia 85 alizoshinda rais Magufuli, sio kwamba tuu anachukua nafasi hiyo kwa awamu nyingine bali pia Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeweka historia kwa kuwashinda wapinzani nguli kwa asilimia kubwa.
Viongozi mashuhuri wa chama kikuu cha upinzania Tundu Lissu ambae alikuwa anagombea kiti cha urais amekosa huku Freeman Mbowe akipoteza nafasi yake ya ubunge kwa kushindwa na mgombea wa CCM.
Pia kiongozi mwingine wa upinzani Zitto Kabwe hakuweza kurudisha nafasi yake ya ubunge.
Rais Magufuli ameendelea kuwaalika wawekezaji kutoka nje ikiwa ni mwendelezo wa juhudi za serikali yake katika kukuza uchumi wa taifa na watanzania kwa ujumla.
Amewataka wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo uchimbaji wa madini.
Raisi Magufuli anatarajia kuapishwa kesho jijini Dodoma.