Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ametoa tamko la kusisitiza matumizi sahihi ya uvaaji wa barakoa kwa kila abiria anaetumia usafiri wa umma.
Aidha amewataka wamiliki wa vyombo hivyo kuwaelekeza madereva na makondakta kuepuka kubeba abiria asievaa Barakoa.
RC Makalla ametoa msisitizo huo wakati wa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kilichoketi kupitia tathimini ya utekelezaji wa mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya juu ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19 na kuendelea kusitiza suala la kutosimamisha abiria (level seat).
Makalla amesema kumekuwa na ulegevu wa usimamizi kwenye baadhi ya maeneo ambapo ametoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Wilaya na LATRA kuhakikisha wanasimamia ipasavyo mwongozo wa Wizara ya Afya.
Kutokana na changamoto za usafiri kwa wanafunzi, RC Makalla ameruhusu daladala kubeba wanafunzi angalau watano watakaosimama wakiwa wamevaa barakoa.
RC Makalla ameendelea kusisitiza wananchi kuepuka mikusanyiko isiyokuwa na lazima na kama ikitokea kuna ulazima taratibu zote za kujikinga zizingatiwe.
Akizungumzia suala la chanjo amesea amefurahi kuona wananchi wamekuwa na mapokeo makubwa ya kupokea chanjo ambapo kwa mujibu wa Mganga mkuu wa mkoa huo adi kufikia Jana tayari Wananchi 10,000 wamefanya wamejiandikisha kupata chanjo na wanahofia huenda chanjo hizo zitawahi kumalizika.