Home BIASHARA Bei holela Zanzibar kudhibitiwa

Bei holela Zanzibar kudhibitiwa

0 comment 110 views

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewahakikishia wananchi kuwa, bidhaa muhimu kama vile mchele, unga wa ngano na sukari hazitokuwa zikipanda bei bila mpangilio kwa kuwapunguzia ushuru wafanyabiashara wa bidhaa hizo.

Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mohamed Hafidh, amesema kuwa licha ya serikali kwenda sambamba na Sera ya biashara huria ambayo inawaruhusu wafanyabiashara kuagiza bidhaa muhimu za vyakula, serikali itaendelea kuhakikisha wafanyabiashara hao hawapandishi kiholela bei ili kuwapa urahisi wananchi ambao wananunua bidhaa hizo kwa wingi.

“Sioni sababu ya wafanyabiashara kupandisha bei ya bidhaa muhimu ikiwemo mchele,unga wa ngano, na sukari kwa sababu bidhaa hizo tumepunguza ushuru wake ili zitoe nafuu kwa wananchi wetu”. Amesema Naibu Waziri huyo.

Pia Naibu Hafidh ameelezea kuwa, serikali imeunda tume maalum kwa ajili ya kumlinda mlaji na moja ya kazi ya tume hiyo ni kuangalia bei za bidhaa za vyakula zinazotumiwa na wananchi hasa vyakula, hivyo bei zikiwa za kawaida mwenendo wa kimaisha wa wananchi utakuwa kawaida na malalamiko yatapungua.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter