Bei ya petroli na mafuta ya taa imepanda kuanzia Novemba 04.
Kwa mkoa wa Dar es Salaam Petroli imeongezeka kwa Sh25 huku mafuta ya taa yakiongezeka kwa Sh12 kwa lita moja.
Kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi mkuu wa Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) Godfrey Chibulunje amesema kwa upande wa kanda ya Kaskazini bei ya petroli imeongezeka kwa Sh52 huku ya dizeli ikipungua kwa Sh38 na mafuta ya taa kwa Sh7.
Mikoa ya Kusini petroli imeongezeka kwa Sh10 na dizeli imepukua kwa Sh83.
Amesema mabadiliko hayo ya bei yametokana na mabadiliko yaliyopo katika soko la dunia pamoja na gharama za ushafirishaji.