Home BIASHARA Bei ya petroli yashuka, dizeli yapanda

Bei ya petroli yashuka, dizeli yapanda

0 comment 104 views

Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza kupungua kwa bei ya petroli kwa Sh31 kwa lita moja mwezi Januari huku bei ya dizeli imeongezeka kwa Sh9 na mafuta ya taa ikipanda kwa Sh29 kwa lita moja.

Mabadiliko ya bei hizo za jumla na rejareja ni kwa mafuta yaliyopokelewa katika Bandari ya Dar es Salaam ambapo yametokana na kinachoendelea katika soko la dunia na gharama za usafirishaji.

Kwa mujibu wa Ewura, bei ya jumla ya petroli imepungua kwa Sh 31.1, dizeli imeongezeka kwa Sh 8.74 na mafuta ya yaa yakiongezeka kwa Sh 29.31 kwa lita moja.

Bei hizo mpya zitaanza kutumika kuanzia kesho Januari 7.

Kutokana na hali hiyo, Ewura imesema kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta kwa kuzingatia bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewana kanuni iliyopitishwa.

“Pia vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei katika mabango yanayoonekana bayana yakiwa na punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika,” ilieleza taarifa hiyo.

Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani. Ewura imesema ni kosa kuuza mafuta bila kuweka bango la bei linaloonekana vizuri kwa wateja.

Ewura imesema adhabu kali itatolewa kwa kituo ambacho hakitatekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni ikiwemo kutotoa risiti za kieletroniki.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter