Home BIASHARA EFD feki zashika kasi, TRA yatoa onyo

EFD feki zashika kasi, TRA yatoa onyo

0 comment 317 views

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere amesema baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakitumia mashine za EFD feki (Ghost machine) kutoa risiti kwa wateja, jambo ambalo linaikosesha serikali mapato stahiki. Kachere amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa washauri wa kodi na kueleza kuwa, ni kinyume na Sheria kutumia mashine hizo zinazotoa risiti zenye viwango vidogo vya kodi huku akisisitiza kuwa ni uhujumu uchumi.

“Tumebainisha wako baadhi ya wafanyabiashara wanafanya mauzo ya Shilingi 800,000, lakini wanatoa risiti ya Shilingi 500,000 au chini ya hapo. Lengo ni kukwepa kodi. Hii si sahihi kabisa na wanahujumu uchumi”. Ameeleza Kachere.

Pamoja na hayo, Kamishna huyo pia amesema kuwa wameshaanza kuchukua hatua kwa wale wanaofanya uhujumu kwa mtindo huo huku akiwaonya washauri wa kodi ambao wamekuwa na tabia ya kuwasilisha marejesho yasiyo sahihi kuwa, taratibu za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

“Katika ukaguzi wetu tulimkuta mhasibu mmoja ana vitabu vitano ambavyo vyote kwa mwaka mmoja vina hesabu tofauti. Cha mauzo ya Sh. Bilioni 142, kingine bilioni 80, na kinachokuja TRA ni Shilingi bilioni 18”. Amesema Kamishna huyo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter