Home BIASHARA Maonyesho ya biashara: Unachotakiwa kufahamu

Maonyesho ya biashara: Unachotakiwa kufahamu

0 comment 129 views

Siku zote maonyesho ya kibiashara huchangamkiwa sana na wafanyabiashara na wajasiriamali kwa ujumla kwa sababu, wakati wa maonyesho mfanyabiashara hupata fursa ya kuonyesha bidhaa au huduma yake kwa watu binafsi na wataalamu mbalimbali hivyo kupata elimu, mawazo mapya na vilevile watu wakinunua bidhaa husika basi mfanyabiashara huyo hunufaika pia na kipato.

Kawaida maonyesho ya kibiashara huandaliwa na kampuni fulani au sekta fulani kwa ajili ya kuonyesha bidhaa zinazohusu huduma au bidhaa zao. Kwa mfano serikali huandaa maonyesho ya nane nane kwa ajili ya wakulima nchini kuonyesha bidhaa zao na hata kujipatia elimu zaidi na vilevile fursa mpya.

Kabla ya kushiriki katika maonyesho haya, mfanyabiashara hushauriwa kujua maonyesho hayo yanahusu nini na kauli mbiu yao. Ili kuamua kufanya maandalizi ya bidhaa zinazohitajika au huduma katika maonyesho hayo au kutokwenda katika maonyesho hayo kwani lengo la maonyesho ni kuhakikisha watu wote wanaohudhuria wananufaika kwa namna moja au nyingine.

Ni muhimu kujua gharama za ushiriki katika maonyesho hayo ili kuepuka kupata hasara. Hivyo mfanyabiashara anatakiwa kutafakari kama akishiriki maonyesho hayo atapata faida au atapata hasara hivyo kuamua kulipia au kutolipia gharama za ushiriki katika maonyesho hayo.

Vilevile mshiriki wa maonyesho ya kibiashara anapaswa kujua eneo la tukio, nikimaanisha eneo ambalo maonyesho hayo yatafanyika ili kufanya maamuzi kuhusu utengenezaji wa miuondombinu katika eneo hilo kwa ajili ya bidhaa au huduma yake, na namna ya kufika katika eneo hilo na biashara husika.

Maonyesho ya biashara ni muhimu kwa wafanyabiashara kwa kuwa kupitia maonyesho hayo, mfanyabiashara hupata fursa ya kuonyesha bidhaa au huduma yake kwa watu wengi hivyo kujipatia wateja wapya, wataalamu wanaoweza kukuza zaidi biashara hiyo.

Pia kupitia maonyesho hayo, ni rahisi kwa mfanyabiashara kutambua mapungufu kuhusu biashara yake na kujifunza zaidi kwa washindani wake.

Kwa ujumla, maonyesho ya kibiashara humsaidia mfanyabiashara kugundua fursa mpya za uwekezaji na pia mfanyabiashara huongeza mtandao wa kibiashara na kufanya majadiliano na wafanyabiashara wengine kwa lengo la kuimarika zaidi kiuchumi na kukabiliana na changamoto za kibiashara.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter