Home BIASHARA Faini milioni 20 kuingiza, kusafirisha mifuko ya plastiki

Faini milioni 20 kuingiza, kusafirisha mifuko ya plastiki

0 comments 239 views

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi na Hifadhi ya Mazingira (NEMC) Dk. Samuel Gwamaka amesema watakaopuuza agizo la serikali na kuingiza ama kusafirisha mifuko ya plastiki watapigwa faini ya Sh. 20 milioni.

“Uingizaji nchini wa mifuko ya plastiki faini ni Sh. 20 milioni, usafirishaji nje ya nchi wa mifuko ya plastiki ni milioni 20; uzalishaji, uhifadhi na usambazaji wa mifuko hii ni Sh. 10 milioni uuzaji wa mifuko ya plastiki ni Sh. 10,000 na utumiaji wa mifuko ya plastiki ni Sh. 30,000”. Amesisitiza Dk. Gwamaka.

Pamoja na hayo, Mkurugenzi huyo ameainisha mifuko mbadala kuwa ni ile ambayo imetengenezwa na karatasi, vikapu, nguo na gunia huku akieleza kuwa aina hizo ni rafiki zaidi kwa afya ya watumiaji na vilevile mazingira.

“Vilevile kuna wawekezaji na wamiliki wa viwanda ambao walikuwa wanasubiri tamko la serikali ili wawekeze mara moja katika utengenezaji wa mifuko mbadala”. Ameongeza Dk. Gwamaka.

Aidha, Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa watanzania wabunifu kuchangamkia fursa ya kutengeneza mifuko mbadala na kuwataka kuwasiliana na taasisi za fedha, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Shirika la Maendeleo la Viwanda Vidogo (SIDO), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na NEMC.

“Serikali inatoa wito kwa wadau wote ikiwemo wawekezaji katika viwanda kuzingatia umuhimu wa uchumi wa mbadala wa mifuko ya plastiki, kwani utaibua ajira nyingi zaidi na kukuza kipato cha wananchi wa kawaida hasa kina mama katika kutengeneza mifuko mbadala ambako kunahitaji teknolojia rahisi na nguvukazi”. Amesema Dk. Gwamaka.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!